Utafiti: Kirusi cha corona chagundulika kwenye maji machafu Uholanzi


Watafiti nchini Uholanzi wanasema kuwa vijidudu vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 vilikuwemo kwenye mfumo wa maji machafu wa mji mmojawapo wa nchi hiyo, wiki kadhaa kabla ya wagonjwa wa kwanza wa kirusi cha corona kuthibitishwa kwenye mji huo.

Taasisi ya Utafiti wa Maji ya KWR ilipima maji machafu kwenye miji saba ya Uholanzi, ambapo sampuli kutoka kinu cha maji cha Amersfoort, karibu na mji wa Utrecht, zilionesha kuwa kirusi hicho kilikuwemo tarehe 5 Machi, muda ambao hata wagonjwa wa corona walikuwa hawajagunduliwa kwenye mji huo

Nchini Uholanzi,wagonjwa wa kwanza wa COVID-19 walithibitishwa tarehe 27 Februari. Uchunguzi wa maji machafu awali ulikuwa ukifanyika kugunduwa uwepo wa kirusi cha polio na matumizi ya madawa katika jamii. Ila huu ni utafiti wa kwanza unaolenga kujuwa uwepo wa kirusi cha corona.