Loading...

5/23/2020

Boris Johnson ashinikizwa amfute kazi mshauri wake mkuu


Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anakabiliwa na shinikizo la kumfuta kazi mshauri wake mkuu baada ya ripoti kuibuka kuwa alikiuka vikwazo vya usafiri.Magazeti ya The Guardian na Mirror yameripoti kuwa Dominic Cummings alisafiri kutoka mjini London hadi Durham kwa wazazi wake licha ya kuonyesha dalili za virusi vya Corona.

Haya yanajiri wiki moja tu baada ya serikali kuweka vikwazo vya usafiri ili kukabiliana na kasi ya maambukizi ya virusi vya Corona.Safari zinaruhusiwa tu kwa dharura huku watu wenye dalili za ugonjwa wa Covid 19 wakitakiwa kujitenga kama tahadhari kwa angalau siku saba.

Hata hivyo, msemaji wa serikali alikataa kuzungumzia tukio hilo.Kiongozi wa chama cha kitaifa cha Scotland Ian Blackford aliandika kwenye mtandao wake wa Twitter akimtaka mshauri huyo wa waziri mkuu ajiuzulu.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger