Idadi ya wasio na makazi kuongezeka nchini Marekani

Imeripotiwa kwamba idadi ya wasio na makazi inaweza kuongezeka kwa asilimia 45 kutokana na athari mbaya ya maambukizi ya virusi vya corona katika uchumi nchini Marekani.

Katika utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Columbia, imesisitizwa kwamba kulipuka kwa Kovid-19 kumesababisha mamilioni ya watu kupoteza kazi zao, jambo litakalosababisha kuongezeka kwa idadi ya wakaazi wa mitaani.

Katika utafiti huo, kulingana na rekodi rasmi za Januari 2019, watu elfu 568 kote Marekani walikuwa wakiishi bila makazi, na kwa sababu ya Kovid-19, imeonywa kuwa idadi hii inaweza kuongezeka  kuwa zaidi ya elfu 250 mwaka huu.