Kamati ya ALAT Pwani yatembelea miradi ya ujenzi wa machinjio ya kisasa Kibaha

KAMATI ya jumuiya ya umoja wa serikali za mitaa ALAT Mkoa wa Pwani imewaagiza watendaji na watumishi wa halmashauri kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano kwa  kuweka mipango madhubuti ambayo itasaidia  kusimamia miradi mbali mbali ya maendeleo ili iweze kukamilika kwa muda uliopangwa bila ya kucheleweshwa kwa maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Hayo yalibainishwa  na Mwenyekiti wa Alat Mkoa wa Pwani  Hatibu Chaulembo wakati wa ziara ya kutembelea miradi mitatu ya kimikakati ikiwemo ujenzi wa machinjio ya kisasa, ujenzi wa soko, pamoja na kiwanda cha kuzalisha dawa ya kuulia mazalia ya mbu  viuwadudu ilivyopo katika halmashauri ya Mji Kibaha na kuongeza kuwa wameridhishwa na hatua ambayo imefikia.

Aidha Mwenyekiti huyo alisema kwamba serikali ya awamu ya tano imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo hivyo inatakiwa isimamiwe ipasavyo na kukamilika kwa wakati ili kuweza kuwasaidia wanannchi wa maeneo mbali mbali katika Mkoa wa Pwani waweze kupata fursa za ajira na wengine kujiajiri wao wenyewe.

“Sisi kama kamati ya Alat Mkoa wa Pwani tumefanya ziara ya kukagua na kutembelea miradi mitatu ya kimikakati katika halmashauri ya mji Kibaha ikiwemo Soko kubwa la kisasa, ijenzi wa machinjio ya kisasa pamoja na kujionea shughuli mbalin mbali za uzalishaji amabzo zinafanyika katika kiwanda cha viuadudu hivyo kwa pamoja tumerudhishwa na mwenendo mzima japo kuna mambo mengine yanatkiwa yafanyiwe kaza zaidi,”alisema Chaurembo.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Musa Gama ambaye pia ni Katibu wa Alat Mkoa wa Pwani alimshukuru Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli kwa kutenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa miradi mbali mbali ambayo itaweza kusaidia kwa kiwango kikubwa kuwasaidia wananchi kujikwamua kiuchumi na kuondokana na wimbi la umasikini.

Gama alibainisha kuwa utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo ni njia moja wapo ya kuwaondolea wananchi wimbi la umasikini hivyo juhudi ambazo zinafanywa na serikali ya awamu tano chini ya usimamizi mzuri waRais Dk. John Pombe Magufuli hivyo kumamilika kwa miradi hiyo kutakuwa ni chachu kubwa katika kukuza uchumi wa nchi.

“Mimi kama Katibu wa Alat Mkoa wa Pwani naweza kusema nimejifunz amambo mbali mbali katika ziara hii amabyo tumeifanya katika halmashauri ya mji wa Kibaha kwani nimeweza kujionea ujenzi wa machinjio makubwa ya kisasa pamoja na soko jipya ambayo hivi vyote kwa pamoja vitaweza kuleta mabadiliko chanya kwa wananchi pindi vitakapokuja kukamilika kw ahiyo ni hatua kubwa sana ambayo imefanyika,”alisema Gama.

Nao baadhi ya wajumbe wa kamati YA Alat Mkoa wa Pwani akiwemo Hamisi Dipakutile, Mshamu Munde pamoja na Jenipher Omolo alisema kwamba serikali ya awamu ya tano imeweza kufanya mambo mengi katika sekta mbali mbali hivyo wana imani kuwa katika siku za usoni miradi hiyo pindi ikikamilika italeta maendeleo makubwa kwa wananchi.