Trump amfukuza kazi Mkaguzi Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje

Rais wa Marekani Donald Trump amemfukuza kazi mkaguzi mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje Ijumaa jioni.

Kufukuzwa kazi kwa Steve Linick usiku ni hatua ya karibuni ya rais kumfukuza kazi msimamizi wa serikali.

Hadi sasa Trump amewafukuza kazi wasimamizi watatu baada ya kutokutwa na hatia na Baraza la Seneti katika kesi aliyofunguliwa na Baraza la Wawakilishi ya kutumia madaraka vibaya na amekuwa akiwakosoa wengine.

Rais alisema katika barua aliyomtumia Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi Ijumaa usiku kuwa “hana tena” kwa hali ilivyo “imani kamili” na Linick.

“Kitendo cha Raischa usiku sana wikiendi kumfukuza kazi Mkaguzi Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje kimeongeza kasi mwenendo wake hatari wa kulipiza kisasi dhidi ya wafanyakazi wa umma ambao wana uzalendo waliopewa majukumu ya kusimamia taasisi hizi kwa niaba ya wananchi wa Marekani,” Pelosi amesema katika tamko lake Ijumaa.

“Mkaguzi Mkuu Linick ameadhibiwa kwa kuenzi kutekeleza jukumu lake kuilinda Katiba na usalama wa taifa letu, kama anavyotakiwa kufanya hivyo na sheria ya nchi hii na kiapo chake.

Mwakilishi Elliot Engel, mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Baraza la Wawakilishi katika tamko lake amesema ofisi yake ilikuwa tayari imepata taarifa kuwa Ofisi ya Mkaguzi Mkuu ya Wizara ya Mambo ya Nje ilikuwa imefungua uchunguzi juu ya Waziri wa Mambo Nje Mike Pompeo.

Kufukuzwa kazi kwa Linick katikati ya uchunguzi huu kunaonyesha wazi kuwa kitendo hiki cha ulipizaji kisasi ni kinyume cha sheria,” Engel alisema katika tamko lake.

Linick was appointed to the inspector general post by President Barack Obama.
Linick aliteuliwa kuwa Mkaguzi Mkuu na Rais Barack Obama.

Kushiriki kwa Linick katika mchakato wa kesi ya kumuondoa madarakani rais uliishia katika kutoa muhtasari kwa kamati mbalimbali za bunge na kuwapatia wabunge nyaraka kutoka kwa mwanasheria wa rais, Rudy Giulian.