Wasanii wanamchukia Diamond sababu ya mafanikio yake- Romy Jons

DJ rasmi wa msanii Diamond Platnumz, Romy Jons maarufu RJ ambaye pia ni kaka wa mkali huyo amedai kuwa baadhi ya wasanii wamekuwa wakimchukia Diamond kutokana na mafanikio aliyokuwa nayo.

RJ ameeleza hayo kwenye kipindi cha Salama na yahstonetown cha EATV ambapo amesema pia tabia ya Diamond ya kutopenda kutoka imefanya wasanii wenzake kuona anaringa.

“Sidhani kama shabiki wanamchukia Diamond Platnumz. Wasanii wenzie wanamchukia sababu ya mafanikio yake aliyokuwa nayo na ile tabia yake ya kukaa nyumbani kutokwenda huku na huko wanaona kama anaringa lakini yeye anapenda tu kukaa nyumbani,” amesema Romy Jons.

Ikumbukwe kuwa, Diamond ni kati ya wasanii waliofanikiwa sana kwenye muziki na kuweza kufungua lebo yake ya Wasafi Classic Baby (WCB) ambayo tayari ina wasanii ambao wanafanya vizuri Kimataifa na kubwa zaidi kufungua "Media House" ambayo ni Wasafi Media