https://monetag.com/?ref_id=TTIb B Dozen afunguka kwa mara ya kwanza baada ya kuhamia EFM | Muungwana BLOG

B Dozen afunguka kwa mara ya kwanza baada ya kuhamia EFM

Aliyekuwa mtangazaji wa Clouds FM, Hamis Mandi maarufu kama B Dozen ambae leo June 3, 2020 ameingia katika vichwa vya habari baada ya kuhamia kituo kipya cha kazi kiitwacho EFM kinachomilikiwa chini ya Mkurugenzi, Majizo.

Mtangazaji huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameyaandika maneno ya kuushukuru uongozi wa Clouds Media Group na kusema…’Kutoka Arusha, Kitega Uchumi hadi Mjengoni Mikocheni, CLOUDS has always been home,Shukrani sana kwa Management yote, Chama la Wana XXL na wafanyakazi wote wa Clouds, na wadau wengine wote wa Clouds Undugu wangu na ninyi hauwezi kuisha wala Kusahaulika’- B Dozen

It is time, nahitaji changamoto mpya mahali pengine.
.
Mwisho ninamnukuu #RugeMutahaba, aliwahi kusema " "Kubadilisha mfumo wa mazingira ya utafutaji na kukua kitasnia nadhani halitakiwi kuwa jambo baya isipokuwa ni kupongezana na kutakiana kila la kheri".
.
I wish you all the best, mzidi kufungua Dunia. 💙💙🙏🏼