https://monetag.com/?ref_id=TTIb Faida za kunywa chai nyakati za asubuhi | Muungwana BLOG

Faida za kunywa chai nyakati za asubuhi


Wapo baadhi ya watu wao wasiponunywa chai kwao huwa ni changamoto sana katika jinsi ambavyo siku yako itakavyokuwa. Wapo baadhi ya watu wao wasipokunywa chai basi huumwa na kichwa siku nzima.

Je, ni mara ngapi umekuwa ukiondoka kwako asubuhi bila kunywa chai? naamini inaweza kuwa ni mara kadhaa lakini wengine ikawa ndio desturi yao kabisa kutokunywa chai asubuhi wanapotoka nyumbani kuelekea kwenye mishughuliko au masomo yao.

Sasa leo ninazo hizi faidia kadhaa za kunywa chai wakati wa asubuhi kabla hujatoka kwako.

1. Husaidia kuongeza uwezo wako wa kufikiria. Hivyo kama wewe ni mwanafunzi au mfanyakazi ni vyema kuzingatia unywaji wa chai kabla ya kuanza shughuli zako za siku husika ili uweze kuongeza uwezo wako wa kufikiri.

2. Unapokunywa chai unajipunguzia hatari ya kuzongwa na magonjwa mbalimbali hususani yale ambayo si ya kuambukiza.

3. Pia unapokunywa chai asubuhi husaidia kuboresha mahusiano mazuri kati yako na familia yako. Kwa sababu unapoamka na kukaa meza moja na watoto au mke au ndugu na kunywa chai huwezesha wanafamilia kujuzana machache kuhusu siku hiyo kabla ya upilika 'ubuys' wa siku hiyo kuanza.

Angalizo; Unapopika chai epukana na kuweka majani mengi na sukari nyingi kwani chai yenye majani na sukari nyingi  yana madhara makubwa sana katika afya.