Faida zitokanazo na ulaji wa matango



Ikiwa watu wengi tunakula tango bila kujua faida zake katika maisha ya kila siku. Watu wengi tunapenda matunda fulani kwa ladha yake tuu bila kutaka kupata faida katika mwili, siku ya leo tutajifunza faida zitokanazo na kula tango.

Hizi ni faida za tango katika mwili wa binadamu na kiafaya;

1. Tango ni chanzo kizuri cha vitamin B.

2. Tango huupa mwili na vitamin kwa asilimia 95 maji kuusaidia kuondoa sumu mwilini.

3. Tango pia hutumika kwenye matunzo ya ngozi/urembo ambapo huwekwa machoni na kuondoa vimbe hasa kwa watu ambao umri umeanza kusogea pia lina silicon na sulfur ambazo husaidia ukuwaji wa nywele.

4. Tunda hilo lina virutubisho kama lariciresinol, pinoresinol na secoisalariciresinol ambavyo husaidia kupunguza aina mbalimbali za kansa kama kansa ya matiti, kansa ya mifuko ya mayai kwa wanawake, kansa ya kizazi kwa wanawake na kansa ya tezi dume kwa wanaume.

5. Pia husaidia kuondoa harufu mbaya kinywani.

6. Tango huondoa hangover kwa watumiaji wa pombe kwani pia hupunguza ukali wa maumivu ya kichwa pale unapoamka asubuhi ila unatakiwa kula kabla ya kulala ili uamke ukiwa vizuri.

7. Husaidia kupungua uzito na mmeng’enyo uende vizuri, kiasi kidogo cha sukari kilichopo kwenye tango na kiasi kikubwa cha maji, tango ni tunda sahihi kukusaidia upungue uzito. Kamba kamba zake huusaidia mwili kuondoa sumu katika mfumo wa chakula na kusaidia mmeng’enyo wa chakula.

8. Tango husaidia wagonjwa wa kisukari, hupunguza mafuta mafuta kwenye mishipa ya damu na huweza kudhibiti shinikizo la damu aina zote mbili (Low and high blood pressure). Tango lina hormone ambayo huhitajika kwenye chembechembe za kongosho (pancreatic cells) ilikuweza kutengeneza insulin ambayo husaidia kudhibiti kiwango cha sukari kwenye mwili hivyo kuwasaidia wagonjwa wa kisukari.

9. Husaidia afya ya viungo, huondoa gout na ugonjwa wa baridi yabisi (Arthritis). Tango ni chanzo kizuri cha silica ambayo inafahamika kusaidia afya ya viungo kwa kuimarisha viunganishi vya viungo (connective tissue). Pia tango lina Vitamin A, B1, B6, C & D, Folate, Calcium, Magnesium na potassium ambavyo hufanya tango linapochanganywa na juice ya karoti huweza kutibu gout na baridi ya yabisi (arthritis) kwa kupunguza kiwango cha tindikali kwenye mkoo (Uric acid).

10. Tunda hili husaidia kupunguza homa pale inapopanda.
Zingatia Madini ya Potassium yanayopatikana katika matango ndicho chakula cha moyo kwa sababu huwezesha moyo kupiga mapigo katika hali ya kawaida.