Hussein Ibrahim Makungu ajitoa katika kinyanganyiro cha kuwania nafasi Urais wa Zanzibar kisa hiki hapa



Na Thabit Madai,Zanzibar.

Hussein Ibrahim Makungu alimaarufu BHAAH amekuwa Mgombea wa kwanza kati ya wagombea 32 kujiondoa katika mbio za kuwania nafasi ya kuteuliwa kuchaguliwa kuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM.

Bhaah ambaye pia ni mwakilishi wa jimbo la Mtoni Unguja amejiondoa katika kinyanganyiro hicho kwa kile ambacho amedai kuwa anapisha  mchakato uendelee kwa kupisha wagombea ambao wanasifa zaidi yake kuendelea  na mchakato huo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Bhaah amesema kwamba sifa za kugombea anazo ndo maana amejitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi hizo ila amekaa na kutafakari kwa kina na kuona kuwa awapishe wagombea wengine ambao ambao wanasifa za kumzidi.

“Leo nmekuja na hizi fomu kwa lengo la kurejesha ila nilipofika hapo juu nmekuta wagombea wengi wamerejesha na wanasifa zaidi yangu hivyo najitoa na kusubiria atakae chaguliwa kumuunga mkono kwa moyo wangu wote,”alisema Bhaah.

Aidha alisema kwamba ameamua uwamuzi huo wa kujitoa na nguvu zote anazipeleka katika kugombea nafasi ya uwakilishi jimboni ambapo bado anamenbgi ya kuyafanya ambayo hajayakamilisha.

“Katika jimbo langu nimefanya mambo mengi lakini sijakamilisha hivyo najiondoa katika nafasi hii kubwa na kuelekeza nguvu katika nafasu ya Uwakilishi ambapo natangaza nia ya kugombea,”alisema Bhaah.