Kocha Mkuu wa Yanga aipongeza simba kwa kuwa mabingwa


Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amewapongeza Simba kwa kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa mara ya tatu mfululizo.

Eymael raia wa Ubelgiji amesema wanaendelea kujiandaa na kuwekeza nguvu na akili zao zote kuhakikisha wanabeba ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports pia kushika nafasi ya pili Ligi Kuu Bara.