Maandamano kukemea matumizi ya nguvu ya jeshi la Polisi , kifo cha Adama Traore na George Floyd yafanyika nchini Ufaransa.
Adama Traore ni kijana mfaransa mwenye asili ya Afrika ambae alifariki mikononi mwa polisi mwaka 2016 nchini Ufaransa.
Traore alikuwa akiwa na umri wa miaka 24, maandamano yamefanyika nchini Ufaransa pia kukemea mauaji ya George Floyd nchini Marekani.
Licha ya marufuku ya kuandamana mjini Paris, waandamanaji wamemiminika mabarabarani karibu na karsi ya sheria wakidai haki itendeke kwa watu wote wakikemea mauaji ambayo husababishwa na matumizi ya nguvu ya maafisa wa jeshi la Polisi.
Wanafamilia ya Adama Traore wameomba haki itendeke kufuatia kifo cha mwanafamilia wao.
Jeshi la Polisi limekabiliana na waandamanaji takribani 20 000 ambao ilijaribu kuwasamabaratisha kwa kutumia mabomu ya kusababishwa kutokwa na machozi.
Baada ya waandamanaji waliokuwa wakiandamana wakiwa na mabango ambayo yameandikwa "haki itendeke kwa Adama Traore" wamekwnda hadi mbele ya ubalozi wa Marekani .
Mbele ya ubalozi huo wa Marekani, waandamanaji wamekemea mauaji ya George Floyd yaliotokea wiki ilipita nchini Marekani na kuendelea kwa maandamano.
Tangu Mei 25, maandamano hufanyika nchini Marekani kukemea mauaji ya mmarekani huyo mweusi aliofariki mikononi mwa maafisa wa usalama Minneapolis.
Maandamano hayo yamefuatiwa na ghasia na uporaji wa mali na uharibifu.
Kifo cha Adama Traore nchin Ufaransa kilitokea mwaka 2016 , kifo hicho kimefananishwa na matukio ya sasa nchini Marekani.
Ripoti iliotolewa kuhusu kifo cha Adama Traore imefahamisha kuwa kijana huyo alifariki kutokana na matumizi ya nguvu ya maafisa wa jeshi la Polisi ddhidi yake na alifariki ndani ya gari la Polisi alipokuw akipelkwa hospitali.
Kesi kuhusu tukio hilo nchini Ufaransa bado haijafunguliwa .