https://monetag.com/?ref_id=TTIb Maandamano ya kupinga hatua dhidi ya virusi vya corona Senegal | Muungwana BLOG

Maandamano ya kupinga hatua dhidi ya virusi vya corona Senegal

Touba , Senegal.Waandamanaji mjini Dakar walichoma moto matairi na kurusha mawe kwa polisi jana usiku wakati wa maandamano kuhusiana na amri ya kutotembea usiku iliyowekwa karibu miezi mitatu iliyopita kutokana na janga la virusi vya corona.

Ghasia hizo katika mji mkuu wa senegal zinafuatia hatua kama hiyo katika mji mtakatifu wa Touba usiku mmoja kabla, ambako makundi ya watu yalichoma moto gari ya kubebea wagonjwa, wakirusha mawe na kupora mli katika majengo ya ofisi.

Vijana waliingia mitaani baada ya muda wa kutakiwa kutotembea usiku kufika na kupambana na maafisa wa polisi, wakirusha mawe na kuchoma matairi, mkaazi wa eneo la kati la Dakar, ambaye hakutaka kutajwa jina akihofia usalama wake aliliambia shirika la habari la Reuters. Kulikuwa pia na maandamano katika jimbo la Kaolack kusini mwa nchi hiyo, amesema afisa wa eneo hilo.

Senegali imethibitisha karibu kesi 4,000 za maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19, ikiwa ni pamoja na vifo 45.Dakar na Touba , miji ambayo yote ni kituo cha biashara na eneo la ibada, imeathirika zaidi.