https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mombasa yathibitisha wagonjwa 67 huku jumla ya wagonjwa ikifikia 2,474 kenya | Muungwana BLOG

Mombasa yathibitisha wagonjwa 67 huku jumla ya wagonjwa ikifikia 2,474 kenya

Katibu wa Wizara ya Afya Mercy Mwangangi ametangaza Ijumaa kuwa idadi ya waliothibitishwa kuambukizwa ugonjwa wa Covid-19 nchini Kenya imeongezeka na kufikia 2,474.

Akitoa taarifa ya kila ya siku kutoka kwa wizara kuhusu maambukizi mapya, Dkt. Mwangangi amesema watu 3,177 wamepimwa katika kipindi cha saa 24 zilizopita huku 134 wakithibitishwa kuambukizwa virusi vya corona.

Wizara hiyo imeongeza kwamba watu 90, 875 wamefanyiwa vipimo nchini Kenya hadi kufikia Juni 5.

Dkt. Mwangangi amesema kuwa wagonjwa 67 wapya wamegunduliwa katika kaunti ya Mombasa, 31 Nairobi, 15 Busia, watano Machakos, wanne Taita Taveta huku kaunti za Kilifi, Kiambu na Nakuru zikirkedi maambukizi ya watu wawili kila moja.

Watu zaidi wameathirika katika kaunti za Garissa, Kericho na Kajiado.