Mwanamke nchini Uganda ajifungua baada ya miaka 47 ya ndoa


Wakati Safinah Namukwaya alipoolewa na Badru Walusimbi, mkazi wa kijiji cha Nunda huko Lwabenge ,katika kitongoji cha Kalungu mwaka 1996, nia yake kuu ilikuwa ni walau kujifungua mtoto mmoja.

Licha ya kuolewa kwa miaka 24, Namukwaya lakini alikuwa hajabarikiwa na watoto.

Jitihada za kupata mtoto lilianza kuandia kwa mwanaume wa kwanza aliyemuoa mwaka 1973 na kuishi naye mpaka 1987, alikuwa anasumbuliwa na tatizo la uzazi kwa mayai kushindwa kukua ndani ya mfuko wa uzazi.

Mnamo Machi 2019, wakati anatimiza miaka 63, alitembelewa na wataalamu wa afya ya uzazi ' Women's Hospital International and Fertility Centre' huko Bukoto, Kampala na kkufanyiwa uchunguzi na Dkt Edward Tamale Ssali, ambaye alimweleza kuwa anaweza kujifungua licha ya umri wake kuwa umesonga.

Miezi kadhaa baadae, alipata ujauzito na siku ya Alhamisi (Juni 25, 2020), Namukwaya alijifungua mtoto katika hospitali ya mkoa ya Masaka.

Dakitari wa Hpspitali kuu ya wilaya ya Masaka Dk.Herbart Kalema Alifahamisha gazeti la udaku la Red Ppepper kwamba mama huyo alipata matatizo wakati wa ujana wake alipopata mimba lakini walimufanyia upasuaji ambao ulifanyika kimakosa na kusababisha kushindwa kuzaa tena.

Hata hivyo Dk. Kalema ameongeza kwamba mama huyo alifanyiwa upasuaji baada ya kukuta mtoto amezungukwa na maji mengi kabla ya kufikisha miezi tisa za kujifungua, mtoto akiwa na miei minane.

Kulingana na Dk. Kalema hali ya mtoto ni nzuri pamoja na mama yake ila mtoto watamutunza kwa majuma matatau kabla ya kuruhisiwa.