https://monetag.com/?ref_id=TTIb Rais Magufuli akutana na Rais Shein, Ikulu Chamwino | Muungwana BLOG

Rais Magufuli akutana na Rais Shein, Ikulu Chamwino

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 03 Juni, 2020 amekutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein katika kikao cha ndani kilichofanyika Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mohamed Ali Shein, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mzee Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally Kakurwa wakifuraia jambo leo tarehe 03-06-2020 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

 Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mohamed Ali Shein akiangalia akiweka udongo katika jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi za Ikulu na kukagua maendeleo ya kazi ya ujenzi wa ofisi hizo inayofanywa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kupitia shirika lake la Suma JKT.

 Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mohamed Ali Shein akiangalia kibao cha jiwe la msingi la Ujenzi wa Uwekaji Ofisi za Ikulu ya Chamwino.

 Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mohamed Ali Shein
akizungumza na wajenzi kutoka JKT mara baada ya kukagua kazi za Ujenzi wa Ofisi za IKULU.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mohamed Ali Shein Ikulu ya Chamwino Dodoma leo.