Wachezaji wa Simba waungana kupinga ubaguzi wa rangi kwa mtu mweusi baada ya kifo cha George Floyd


Ikiwa nchi mbalimbali zimeonyesha kukerwa na kitendo cha ubaguzi ulitokea Marekani baada Mmarekani mweusi George Floyd kuuawa mikononi mwa polisi na kusabisha nchi mbalimbali kuandamana na kupinga ubaguzi.

Wachezaji wa timu ya simba pia wameonyesha ishara ya kupinga kitendo hicho kilichoondoa uhai waGeorge.

Wachezaji hao walionesha ishara ambayo imetumika sana kipindi hiki na waandamanaji wengi ambapo walipiga magoti kabla ya kuanza mazoezi leo asubuhi ili kupinga ubaguzi wa rangi kwa watu weusi.