Afrika Kusini yavunja rekodi ya kuchukua vipimo vingi zaidi vya corona Afrika kwa siku moja


Jimbo la Gauteng la kaskazini mashariki mwa Afrika Kusini limekuwa kivotu kikuu kipya cha ugonjwa wa corona nchini humo huku maafisa wa afya wa nchi hiyo wakivunja rekodi ya kuchukua vipimo zaidi ya 50 elfu vya corona kwa siku moja.
Taarifa zinasema kuwa maambukizi ya kirusi cha corona ni mabaya na makubwa mno katika jimbo hilo la Gauteng ikilinganishwa na maeneo mengine yote ya bara la Afrika.
Ingawa watu wa afya wanafanya juhudi mbalimbali, lakini kumekuwa na malalamiko ya kutochukuliwa hatua za kweli za kupambana vilivyo na ugonjwa hatari wa COVID-19 nchini humo. Mapema wiki hii, wafanyakazi wa afya wa Afrika Kusini walifanyia uchunguzi vipimo 56 elfu vya COVID-19 kwa siku moja na kufikisha idadi ya watu wote waliochukuliwa vipimo vya corona nchini Afrika Kusini kufikia milioni mbili.