Loading...

Jul 11, 2020

Alikiba, Diamond, Mwana Fa , Billnass na Marioo waunganaWasanii kutoka kiwanda cha BongoFleva Alikiba, Mwana Fa, Billnass na Marioo na baadhi ya wasanii wengine wameonekana wakiwa Jijini Dodoma kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa CCM Taifa 2020

Picha hiyo ikiwaonyesha wasanii hao wakiwa Jijini Dodoma imepostiwa katika ukurasa wa msanii Marioo ambapo ameandika kuwa  "Mkubwa utakuwa umeedit sijawahi kuwa kibonge hivyo sema kimpango wako na editing zako"

Mkutano huo Mkuu wa CCM Taifa 2020 unaofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete ambapo umehudhuriwa na viongozi wa zamani wa nchi kama Rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, Rais wa awamu ya tatu Benjamin William Mkapa na Rais wa Awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.

Viongozi wengine waliokuwepo kwenye Mkutano huo mkuu ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, na Mwenyekiti wa chama cha CUF Prof. Ibrahim Lipumba.

Kupitia Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Humphrey Polepole amesema kuna kazi kama mbili na nusu, kwanza ni kumchagua mgombea wa CCM Tanzania, pili ni kumtambulisha mgombea mwenza wa Jamhuri ya Muungano, tatu ni kumtambulisha mgombea wa Urais wa Zanzibar.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger