Bei ya ufuta yaanza kunona, wakulima meno nje.

 Na Ahmad Mmow, Lindi.



 Bei ya ufuta  i katika chama kikuu cha ushirika cha Lindi Mwambao mkoani Lindi imepanda na kusababisha furaha na matumani kwa wakulima wa zao hilo. Katika mnada wa sita kwa msimu wa 2020 katika chama kikuu cha Lindi Mwambao uliofanyika leo katika kijiji cha Nyangao  bei ya juu kwa kila kilo moja ilikuwa shilingi 1,890 na bei ya chini shilingi 1,840. Bei hizo nitofauti na bei za mnada wa nne katika chama kikuu cha RUNALI ambao bei ya juu ilikuwa shilingi 1,745 na bei ya chini shilingi 1,737 kwa kila kilo moja.

 Huku katika mnada wa tano kwa chama cha Lindi Mwambao  bei ya juu ilikuwa shilingi 1,725 na bei ya chini ilikuwa shilingi 1,720 kwa kila kilo moja. Katika mnada huo wa leo ambao ulihudhuriwa na wakulima wa kijiji cha Nyangao ambao waliridhia ufuta wote uliopo kwenye maghala ya Nangurukuru, Bucco na Mtama uuzwe kampuni za Mahashili, Your home, Export Trading na HS Impex zilinunua tani zote 3395 na kilo 157. Akizungumza baada ya wakulima kuridhia bei hizo, makamo mwenyekiti wa Lindi Mwambao, Rashid Masoud aliwataka viongozi na watendaji wa vyama vya msingi vya ushirika waharakishe kupele  ka taarifa za wakulima ili walipwe mapema kila baada ya mnada kufanyika


Masoud alisema kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wakulima, ambao wanalalamika kutolipwa fedha zao wakati wanunuzi hawacheleweshi malipo. '' Wanunuzi wanaingiza fedha haraka sana, tatizo lipo kwa viongozi na watendaji wa vyama vya kutoshughulikia na kutuma haraka taarifa. Kwamfano chama cha msingi Pachani wakulima wanalalamika hawajalipwa. Matokeo yake tunapakwa matope kwamba Lindi Mwambao tunachelewesha malipo yao.

 Tunaomba ofisi ya mkoa kupitia idara ya ushirika mtupe ushirikiano kutatua tatizo hili,'' alisema Masoud. Nae kaimu mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika wa mkoa wa Lindi, Edmund Masawe licha ya kuhaidi kutembelea vyama vyote vya msingi alitoa wito kwa wakulima washiriki kikamilifu mageuzi ya kiuchumi kupitia ushirika. Huku akiwakumbusha kwamba vyama vya ushirika ni mali yao nasio mali ya viongozi. Lakini pia alitaka minada ifanyike katika maeneo ambayo yana ufuta mwingi ambao haujanunuliwa. Kwani maeneo ambayo wakulima wameuza hayana mahudhurio mazuri ya wakulima minadani.

Kwaupande wa wakulima, walifurahishwa na kupanda kwa bei ya zao hilo. Huku wakiweka wazi kwamba bei zilizopita ziliw Kayanda: akatisha tamaa. Eric Lukanga, mwenyekiti wa Nyangao B alisema bei za awali ziliwakatisha tamaa, lakini kwamwenendo wasasa wamefarijika na wanamatumaini makubwa zitazidi kupanda. Mkulima Maria Mpili, yeye alitoa wito kwaserikali isimamie na kuvisukuma vyama vya msingi vya ushirika viandae taarifa haraka ili wakulima walipwe haraka. Huku nae pia akiunga mkono maelezo ya Lukanga.