Je Wajuwa Faida Zipatikanazo Kwa Kiumbe Mdudu Mende?

Mjue Mende
1.Ni mdudu anayeweza kuishi zaidi ya mwezi bila ya kula chakula chochote. Wana uwezo wa kuishi katika mazingira magumu. Aina moja kwa jina Eublaberus posticus wanaweza kuishi mwaka mmoja kwa kunywa maji pekee.

2.Ni mdudu anayeweza kuishi wiki mbili bila ya kunywa maji.

3.Wakati moyo wa mwanadamu ni mmoja wenye chemba nne mende ana moyo mmoja wenye chemba kumi na tatu.

4.Baadhi ya mende wa kike hawaitaji wanaume kuweza kuzalisha mayai hupandana wao kwa wao na kutaga mayai katika kipindi chote cha maisha yao.

5.Mende ana uwezo wa kukaa kwa zaidi ya dakika 40 bila ya kupumua.

6.Mende ana uwezo wa kuishi zaidi ya wiki mbili akiwa amekatwa kichwa.

7.Ana uwezo wa zaidi ya mara 15 ya binadamu wa kuzuia miale mikali ya nuklia isimdhuru na kubaki hai.

8.Mende ni mdudu asiye na mapafu.

9.Ana uwezo wa kuruka maili 3 kwa saa.

10. Badala ya kuwachukia, wanasayansi huwafurahia sana na kuwatumia kwa manufaa ya binadamu. Mwaka 1999, mende walitumiwa na Prof Robert Full katika Chuo Kikuu cha California, Berkley, kumpa wazo la kuunda roboti ya miguu sita iliyosonga upesi na kwa urahisi.

11. Mende wanatumiwa pia katika matibabu. Wanasayansi kwa miaka mingi wamekuwa wakishangazwa na uwezo wa mende kukaa muda mrefu maeneo yenye sumu na uchafu bila kudhurika.
Wamegundua kwamba huwa wanatoa kemikali za kupigana na sumu. Leo katika hospitali Uchina, krimu inayotengenezwa kwa kutumia ungaunga wa mende waliosiagwa hutumiwa kutibu vidonda vya moto na pia humezwa kutibu vidonda vya tumbo.