Katibu CCM: Mpigieni kura ya dhahabu JPM

KATIBU wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma ,Angelo Madundo amewataka wakazi wa wilaya hiyo kutambua kazi za utekelezaji wa miradi mbalimbali iliyofanywa na mwenyekiti wa chama hicho taifa ambaye pia ni Rais wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli.

 Wito huo ameutoa wakati chama hicho kilipokuwa kikiwapokea wanachama wapya ambao baadhi yao walikuwa ni viongozi wa vyama vya upinzani akiwemo na aliyewahi kuwa diwani wa chama cha Demoklasia na Maendeleo (Chadema)katika kata ya Mbinga B, wilayani humo kutimkia CCM kwa kilekilichodaiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais Dk.John Pombe Magufuli.
Aidha katibu huyo amewataja wengine kuwa ni Gaudensia Komba ambaye alikuwa diwani wa viti maalumu na mwenyekiti wa baraza la wanawake Chadema katika Wilaya ya Mbinga. 

Madundo amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano ifanya mambo mkubwa sana katika utekelezaji wa miradi ya sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya ambapo Zahanati na vituo vya Afya vimejengwa na huduma zinatolewa. 

Amesema kufuatia hali hiyo wakazi wa maeneo mbalimbali wakiwemo wa wilaya ya Mbinga wanatakiwa kuyatambua maendeleo hayo kisha kumuunga mkono Rais Dk.John Pombe Maguli ili azidi kuleta maendeleo zaidi. 

Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mbinga Beda Hyera wakati akiwapokea wanachama hao amesema kuwa katika uchaguzi uliopita wilaya hiyo ilipoteza kata tatu ambazo zilienda upinzani na kuwa uchaguzi huu wa sasa CCM haitapoteza hata kata moja. 

Hyera amesema kuwa chama hicho bado kipo imara hivyo kitaendelea kutekeleza yale yote yaliyoahidiwa kwenye ilani na kuwafanya wananchi waendelee kunufaika na maendeleo hayo ambayo hadi sasa yanaonekana. 

Naye aliyewahi kuwa diwani wa kata ya Mbinga B, kwa tiketi ya Chadema Frank Mgeni wakati akijiunga na CCM amesema kuwa ameamua kujiunga na chama hicho ili kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano.