Loading...

Jul 13, 2020

Kauli ya kwanza ya Shilole toka achezee kipigo kwa mumewe

Mwanamuziki wa bongo na mfanyabiashara Shilole ameibuka tena baada ya siku chache kuposti  picha zikimuonyesha ameumizwa na mumewe baada ya kupigwa na mumewe leo ameibuka na kuwashukuru wa tanzania  kwa ushirikiano kipindi cha matatizo yake.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Shilole aliandika hivi

 Salaam ndugu zangu,

Nimeona upendo, nimeona heshima na kukubalika kwa kiwango cha pekee katika wakati huu wa changamoto niliyokutana nayo.

Nashukuru sana kwa upendo wenu, Nashukuru sana wote walionijulia hali na kuniombea dua.

Kuhusu maendeleo yangu mimi niko sawa, naendelea kupambana. Changamoto ni sehemu ya maisha, haziwezi kunifanya nianguke. Lakini yote hayo sio kwa nguvu zangu, ni Mungu na upendo wa Watanzania wenzangu mnaonitakia mema.

Maisha yanaendelea, tuendelee kuijenga jamii yetu : Jamii itakayokataa kabisa unyanyasaji wa kijinsia.
🙏🏼
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger