Mwaandishi wa habari wa Muungwana Blog Zanzibar anyakua Tunzo 3 za utetezi wa watoto


Mwandishi wa Habari wa Muungwana Blog visiwani Zanzibar,Thabit Hamidu Madai amepata  Tunzo Tatu ya Umahiri wa Uwandishi wa habari Mitandaoni  kwa habari zinazohusu udhalilishaji na ukatili wa watoto visiwani Zanzibar.



Tunzo hizo zimetolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia haki za watoto Duniani (UNICEF) kwa kushirikiana na Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar (WAHAMAZA) na kukabidhiwa na Wazira wa Kazi,Uwezeshaji Wanawake,Wazee na Watoto Zanzibar, Moudline Cyrus Castico.



Hafla ya kukabidhi Tunzo ilifanyika katika Ukumbi wa Jumuiya walemavu Zanzibar uliopo weilesi Kikwajuni na kushirkisha Waandishi wa Habari, Wahariri wa vyombo vya Habari na wadau mbalimbali wa Habari kutoka ndani na nje ya Nchi.



Jumla ya Tunzo 9 zimetolewa ambazo ni Tunzo za Waandishi wa habari bora wa habari za watoto katika vipindi vya Redioni, Makala za magazeti, vipindi vya televisheni na Habari na makala za mitandaoni ambapo Thabit Madai alichukua nafasi kwanza,Nafasi ya Pili na Nafasi ya kwanza katika kundi la Mwandishi wa Habari za mitandao.



Akizungumza Mara baada ya kukabidhi Tunzo hizo, Wazira wa Kazi,Uwezeshaji Wanawake,Wazee na Watato Zanzibar,Moudline Cyrus Castico aliwataka waandishi wa Hbari kuongeza kasi katika kuandika habari zinazohusu changamoto za watoto visiwani humo ili Serikali na wadau mbalimbali kuweza kuzitatua.



“Waandishi wa Habari bado muna kazi kubwa sana ya kuandika hizi changamoto zinazowakabiliwa watoto visiwani Zanzibar ili zitatuliwe na watoto wetu waishi kwa amani, hivyo nawaomba zidisheni kasii hii kwa mashirikiano na Serikali” alisema Waziri Castico.