Mwigizaji wa Marekani Kelly Preston afariki dunia

Mwigizaji wa Marekani Kelly Preston (57) ambaye alifanya vizuri kwenye Filamu za Jerry Maguire, Twins na Mischief amefariki Dunia jana July 12,2020 kutokana na kuugua Kansa ya Matiti, Mumewe John Travolta ambaye pia ni Mwigizaji (Hollywood Star) amethibitisha.

“Kwa moyo wenye majonzi makubwa nasikitika kuwafahamisha kuwa Mke wangu, Kelly wangu mrembo amefariki baada ya kupigana kwa miaka miwili akisumbuliwa na Kansa ya Matiti”-TRAVOLTA