Serikali yazindua mpango wa kuendeleza viwanda vidogo na vyakati hapa nchini


Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.

Serikali kupitia baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchimi NEEC imezindua mpango wa uendelezaji wa viwanda vidogo na vya kati mpango utakaowawezesha wajasiliamali hapa nchini kupata mikopo yenye riba nafuu ili kuendeleza viwanda vyao.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, ajira, vijana na watu wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, amesema mpango huo utakuwa siluhisho la ukosefu wa mitaji kwa wajasiliamali hapa nchini.

" Niwatake wananchi wote wenye wenye vigezo kujitokeza kwa wingi kupata mikopo hii ili kuinua mitaji na kuendeleza ujasiliamali wao" amesema Mhe Jenista.

Ameongeza kuwa " utafiti unaonyesha kuwa kungu kazi kubwa hapa nchini ni vijana lakini changamoto ilikuwa ni ujuzi na mitaji lakini kwa mpango huu watapatiwa mitaji kwa njia ya mkopo ili nao wawe sehemu ya kuchochea kukua kwa uchumi" amesema.

Aidha Mhe Mhagama amezitaka taasisi zinazohusika na mpango huu ambazo ni NSSF, VETA, SIDO na AZANIA BANKI wakiratibiwa na baraza la uwezeshaji wananchi kiuchimi NEEC, kila mtu kusimamia nafasi yake ili kuhakikisha mpango huu unafanikiwa.

Pia ametaka mpango huo uwe shirikishi kwa watanzania wote bila kuwa na ubaguzi na kuhakikisha mikopo hiyo inakwenda kwa wale wenye sifa tu, na kuwataka wasimamizi kuwa waaminifu katika kutekeleza mpango huo.

Amesema kwa awamu hii ya tano kumekuwa na ongezeko la viwanda vingi vikubwa na vidogo jambo ambalo limesaidia kukua kwa pato litakanalo na viwanda kutoka asilimia 8.05 hadi kufikia 8.5 kwa sasa.

" Katika awamu hii kuna viwanda elfu name Mia nne sabini na saba (8477) viwanda vikubwa 201, viwanda vya kati 460, viwanda vidogo 3406, na vidogo kabisa 4410, Sasa kuja kwa mpango huu kutarahisisha kuwa na viwanda vingi zaidi" amesema.

Pia ametaka kutengenezwa kwa mfumo wa kanzi data utakaowezesha kuwafahamu wale wote waliokopa ili iwe rahisi kuwafuatilia katika kujua maendeleo yao, huku akiwataka wawezeshaji kutocheleweshwa kwa mikopo hiyo.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza La taifa la uwezeshaji wananchi kiuchimi NEEC, bi Beng'i Issa, amesema mpango huo utashirikisha taasisi nne ambapo NSSF kama wafadhili, AZANIA BENKI, watakao husika kutoa mikopo.

Wengine ni VETA  ambao watahusika kutoa utambuzi wa mafunzo ya wanufaika wa mikopo na SIDO ambao watahusika katika kutoa ujuzi na Teknolojia kwa wanufaika wa mpango huo.

Kwa muunganiko huo itasaidia katika kutoa ujuzi, elimu na mikopo hiyo utasaidia kupunguza changamoto zilizokuwa zikiwakabili wananchi hususa ni katika mitaji na ujuzi.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa shirika la taifa la hifadhi ya jamii NSSF, William Erio, amesema wao Kama wawezeshaji wa mpango huo tayari wameshatoa bilioni tano(bil 5) kwa ajili ya kuwezesha mpango huo na wataendelea kutoa kadri ya mahitaji ya mpango huo.

Amesema mpango huo utawezesha watanzania kupata mikopo na ujuzi hapa nchini, amesema uwezeshaji wananchi kiuchumi utawezesha kuzalisha bidhaa nyingi na kupunguza uingizaji wa bidhaa za nje hapa nchini.