Vijana wa CCM vyuoni watakiwa kushikamana

 
Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.

Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi taifa Hamfrey Polepole amewataka vijana kushikamana, na kutetea na kuweka bayana mambo mazuri ambayo yamefanyika na serikali hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi ili Rais kupata ushindi wa kishindo.

Polepole ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa mkutano na wanafunzi wa vyuo vikuu wa CCM katika Mkoa wa Dodoma SENETA, amesema kuna mambo mengi yamefanyika katika kipindi hiki Cha awamu ya tano na vijana ni wajibu wao kulinda heshima hiyo.

Amesema vijana inabidi kushikamana na kuyaeleza bayana kwa jamii mambo ambayo yamefanyika ili hata katika uchaguzi wananchi wajue nini kimefanyika na awamu ya tano.

"Vijana ninyi ndio mnaotakiwa kuyasema hayo kwasababu kuna mambo makubwa yamefanyika kubwa na laujasili ni hili la kuhamia Dodoma ndoto ya mda mrefu sasa serikali ipo Dodoma" amesema Polepole.

Polepole amesema chama hicho kwa mapenzi yake kwa wananchi kimetoa mali za chama hicho ikiwamo vyuo walivipeleka serikalini ili vikahudumie watanzania wote wa CCM na wa vyama vingine.

" Ukitaka uamini hiki chama kinajali wananchi wake Kama mlikuwa hamjui Chuo Cha Hombolo ilikuwa Mali ya chama, ukumbi wa Chimwaga, Chuo Cha mwalimu Nyerere, Chuo Cha mahakama Lushoto huo ni mchango wa Chama" amesema.

Amesema kwa mambo ambayo yamefanyika katika awamu ya tano ni wazi kuwa chama hicho kitapata ushindi wa kutosha katika uchaguzi ujao.

Amesema kutokana na Mambo makubwa ambayo yamefanyika na awamu hii umefanya watu kuendelea kukiamini chama hicho ambapo kitakwimu wameongezeka.

" Takwimu za awali zilionesha tulikuwa na wanachama milioni nane (8) lakini kwa Sasa takwimu zinaonyesha tunawanachama milioni kumi na tano (mil 15).

Kwa upande wake Mbunge wa Viti maalumu anayewakilisha vijana Mariam Ditopile, amesema kwa Sasa katika vyuo vingi vimetulia hamna migomo kwa sababu kila kitu kinatekelezwa kwa wakati.

Aidha amewashauri vijana kutodharau ngazi flani kwa kuamini sio saiv yao na kusema nafasi zote katika uongozi ni sawa hamna kazi ndogo na kubwa.

" Unakuta sehemu Kuna kijana anauwezo mkubwa na anaweza kugombea udiwani akapata na kuwa kiongozi wa halmashauri mkubwa lakini hataki anataka ubunge hili sio sahihi kabisa vijana tubadilike" amesema Mariam.

Nae Mwenyekiti wa Umoja wa wanafunzi wa vyuo vikuu wa CCM, Raphael Kunambi amemshukuru Rais Dkt Magufuli kwa kuendelea kuwaamini vijana na kuwateua katika ngazi mbalimbali huku akisema vyuo vyote Mkoa wa Dodoma viko salama kabisa.