Wakili wa ‘tapeli’ Mnigeria aliyejinaji mtandaoni asema FBI ilimteka

Mwanaume mmoja Mnaigeria anayeshutumiwa kwa wizi wa mamilioni ya dola na usafirishaji haramu wa pesa na nchini Marekani alitekwa nyara na FBI, wakili wake amesema.

Ramon Olorunwa Abbas - anayefahamika na wafuasi wake milioni 2.5 kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram kama Ray Hushpuppi - na mshukiwa mwingine wa wizi wa kimtandao Olalekan Jacob Ponle (aka Mr Woodberry) walikamatwa mjini Dubai, ambako wanaishi mwezi Juni.

Baadae walifikishwa katika mahakama ya Chicago tarehe 3 Julai.

Muungano wa miliki za kiarabu (United Aran Emirates) hauna mkataba wa kuwasafirisha wahalifu kwenda Marekani lakini polisi ya Dubai walisema wamekwishwa wasafirisha hadi Marekani.

Msemaji wa Wizara ya sheria nchini Marekani ameiambia BBC kuwa Hushpuppi alifukuzwa kutoka Dubai na hakuletwa Marekani.

Wakili wa Hushpuppi alisema nini?
Wakili wa Abbas, Gal Pissetzky ameiambia BBC kwamba mteja wake , ambaye picha zake kwenye mtandao wa Instagram zilionyesha maisha ya kifahari , hakua mhalifu na alipata pesa kwa njia halali.

"Ana ushawishi katika mitandao ya kijamii akiwa na mamilioni ya wafuasi, akiwa na mamilioni ya watu wanaompenda na kumheshimu, na anawapenda, na hicho ndicho alichokifanya.

Katika jamii ya sasa, hiyo ni biashara," alisema.

Bwana Pissetzky anakiri kwamba hafahamu "kwa 100% " masuala ya mitandao ya kijamii na watoto wake walimwambia kuwa ni mtu mzima sana lakini ana fahamu "hivyo ndivyo watu wanavyotengeneza pesa siku hizi.

Hoja ya wakili wa mshitakiwa wa Chcago ilikuwa kwamba Hushpuppi alilipwa na nembo za mitindo ya mavazi katika kesi hiyo inayotarajiwa kuchukua muda mrefu katika mahakama ya Marekani.

Shirika la upelelezi la Marekani (FBI) linamshutumu Bwana Abbas, mwenye umri wa miaka 37, kwa kuhusika katika wizi wa pesa wa mamilioni ya dola kwa njia ya barua pepe na mifumo mingine ya wizi.

Je Marekani ilitimiza sheria ?

Ni kesi kubwa zaidi ya wizi inayomuhusisha raia wa Nigeria nchini Marekani lakini wakili wake anasema Marekani haina mamlaka ya kumsafirisha kutoka Dubai.

"Kwa maoni yangu, FBI na serikali hapa walivunja sheria walipo mtekanyara kutoka Dubai bila mchakato wowote wa kisheria unaowaruhusu kufanya hivyo ," Bwana Pissetzky toaliiambia BBC.

"Hapakua na mchakati wa kisheria wa kumsafirisha, hapakua na nyaraka za kisheria zilizowasilishwa, likua ni wito wa FBI. Sio raia wa Marekani, Marekani haina kabisa mamlaka ya kumchukua ," alisema wakili wake.

Lakini polisi ya Dubai ilisema katika ujumbe wake wa Facebook kwamba mkurugenzi wa FBI aliwashukuru kwa kuwasafieisha wanaume hao wawili.