https://monetag.com/?ref_id=TTIb Wataalamu wa WHO kuzuru Beijing kuchunguza chanzo cha virusi vya Corona | Muungwana BLOG

Wataalamu wa WHO kuzuru Beijing kuchunguza chanzo cha virusi vya Corona

Wataalamu wawili wa shirika la afya duniani WHO watazuru mji mkuu wa China, Beijing kama sehemu ya kuchunguza chanzo cha virusi vya Corona.

Wataalamu hao, akiwemo wa afya ya wanyama na daktari wa kuchunguza kiini cha magonjwa watakutana na wenzao kutoka China ili kuchunguza jinsi virusi hivyo vilivyotoka kwa wanyama na kuingia kwa binadamu.

Wanasayansi wanaamini kuwa asili ya virusi vya Corona ni wanyama aina ya popo, na baadaye virusi hivyo viliambukizwa kwa wanyama wengine na hatimaye kuwafikia binadamu.

Mji wa Wuhan ndio ulikuwa kiini cha virusi hivyo mwaka jana, lakini uchunguzi wa hivi karibuni umeonyesha kuwa huenda mlipuko huo ulianzia sehemu nyengine.

China imepiga marufuku biashara ya wanyama pori na kufunga baadhi ya masoko nchini humo ili kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo.