Waziri Bashungwa: Watanzania tupendelee bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya hapa nchini kwetu

Wananchi wametakiwa kuendelea kupenda bidhaazinazozalishwa na viwanda vya hapa nchini kwani chanzo cha nchi kufikia uchumi wa kati ni pamoja na wananchi wake kupendelea bidhaa ambazo wanazizalisha wao kama wao.

Akizungumza baada ya kutembelea mabanda ya maonesho ya 44 ya sabasaba katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa amesema kuwa kama watanzania ili kuweza kusheherekea mafanikio endelevu kuingia nchi yenye kipato cha kati tunatakiwa kuwa wakwanza kutangaza bidhaa zetu.


“Kupitia mafanikio tuliyoyapata rai yangu kwa watnzania ni kupenda bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyetu ili mafanikio haya ya kuwa nchi ya kipato cha kati yawe ni matunda kwa watanzania hasa kwa wakina mama wanaotafuta ajira na tukiendelea kupenda bidhaa zinazozalishwa hapa nchini ndivyo tunazidi kutengeneza fursa kwa vijana na wakina mama kupata ajira”. Amesema Mhe.Bashungwa.

Aidha Mhe.Bashungwa amesema kupitia maonesho ya Sabasaba tuendelee kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kupenda bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.

“Kabla haujanunua bidhaa kutoka nje jiulize kwanza nikinunua bidhaa inayotoka nje nikaacha ambayo inazlishwa hapa nchini utakuwa umeinufaisha nchi kwa kiasi gani”. Amesema Mhe.Bashungwa.


Amesema Watanzania tukiendelea kusheherekea mafanikio haya ya kufikia kipato cha kati tuyasheherekee kwa kupenda bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.

Tunategemea kupitia maonesho haya ya sabasaba ya 44 kampuni ambazo zinashiriki ukiondoa wale ambao wanakuja sabasaba kununua bidhaa na kuangalia teknolojia mbalimbali zikioneshwa na taasisi zetu na makampuni pia kupitia B2B wale ambao wapo nje wataendelea kuingia mikataba na wafanyabiashara ambao wanashiriki katika maonesho ya sabasaba na sisi mkakati wetu kama serikali kwasababu ajira nyingi tunazitengeneza ngazi ya viwanda vidogo na vya kati”. Amesema Mhe.Bashungwa.

Pamoja na hayo Mhe. Bashungwa amesema Tanzania kuwa nchi yenye kipato cha kati inatusaidia kuingia kwenye rada ya kimataifa hivyo wengi watapenda kuja kuwekeza hapa nchini.