Mamia wafa’ kwasababu ya taarifa potofu za Covid-19


Mitandao ya kijamii ya Facebook, Twitter na WhatsApp zimeshindwa kukabiliana na kusabaakwa taarifa ghushi kuhusu Covid-19


Takriban watu 800 wamekufa kote duniani kutokana kwasababu ya taarifa potofu zinazohusiana na virusi vya corona katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza ya mwkaa huu, wanasema watafiti.


Utafiti uliochapishwa katika jarida la Marekani linaloandika taarifa za magonjwa ya maeneo yajito na usafi, unasema kuwa watu wapatao 5,800 walilazwa hospitalini kutokana na taarifa zisizo sahihi juu ya corona zilizotumwa kwenye mitandao ya kijamii.

Shirika la Afya Duniani (WHO) awali lilisema kuwa "janga la taarifa" zinazozingira Covid-19 husambaa haraka sawa na virusi vyenyewe, huku nadharia potofu, uvumi na unyanyapaa wa kitamaduni vyote kwa pamoja vikichangia vifo na majeraha

Wengi wa wahanga walifuata taarifa zinazofanana na taarifa za kuaminika za kimatibabu-kama vile ulaji wa kiwango kikubwa wa vitunguu saumu au kunywa kiwangi kikubwa cha vitamin mabli mbali kama njia ya kujikinga na maambukizi, anasema muandishi wa utafiti huo.


Matendo haya yote yalikua na "uwezekano wa kusababisha athari mbaya" kwa afya zao, watafiti wanasema.


Utafiti huo unasema kwamba huo ni wajibu wa mashirika ya kimataifa , serikali na mitandao ya kijamii kupambana na "janga la taarifa potofu",lakini makampuni ya kiteknolojiayamekuwa yakikosolewa kwa kuzorota kujibu taarifa potofu zinapotolewa. Nchini Uingereza sheria za kudhibiti taarifa zenye madhara kwenye mtandao huenda zikawa mbali miaka kadhaa .


Uchunguzi binafsi wa BBC ulibaini kuwa viunganishi(links) za taarifa za matusi, mashambulio ya moto na mauaji kutokana na taarifa potofu juu ya virusi , na kuongea na daktari, wataalamu na wahanga juu ya uzoefu wao.

Post a Comment

0 Comments