Mawaziri wa Uturuki wawasili Lebanon

Makamu wa Rais wa Uturuki Fuat Oktay na Waziri wa Mambo ya nje wa taifa hilo Mevlüt Çavuşoğlu wamewasili mjini Beirut Lebanon wakitokea mjini Ankara.


Viongozi hao wamewasili nchini humo kwa lengo la kutoa msaada baada ya mlipuko wa ghafla uliotokea Beirut.


Oktay, ambaye atakutana na Rais wa Lebanon Michel Aoun, Spika wa Bunge Nebih Berri na Waziri Mkuu Hassan Diyab, anmeabatana na Waziri wa Mambo ya nje Mevlüt Çavuşoğlu.


Mnamo Agosti 4 katika Bandari ya Beirut, moto ulitokea katika ghala namba 12, ambapo milipuko ilianza, na ndipo mlipuko mkubwa sana ukatokea ambao ulitikisa mji wote wa Beirut.


Katika mlipuko huo, watu 154 wamepoteza maisha na takriban watu elfu 5 wamejeruhiwa.

Post a Comment

0 Comments