Sallam sk afunguka sababu ya kukataa kumpa mkono Harmonize

 

Meneja wa WCB, Sallam sk ameeeza ni kwanini alikataa kumpa mkono Harmonize katika mazishi ya mke wa Babu Tale.

Akizungumza na WasafiTV, amesema kuwa alikataa kutokana na Harmonize hakuwahi kumsalimia kwa zaidi ya miaka miwili na amekuwa akikutana naye na hamsalimii.

“Walivyoona lile tukio limetokea kwenye mazishi, wakachukulia kuwa Sallam kachukia kwa sababu Harmonize kaondoka kwenye Lebo, lakini Harmonize hakuwahi kunisalimia kama miaka mitatu iliyopita au miwili, toka yupo WCB,” ameeleza.

“Kwa hiyo sikuona umuhimu wa yeye kuja kunisalimia pale, nishawahi kukutana naye sehemu kibao akaniruka, sikuona umuhimu kwa siku ile kwanini tudanganye umma, na mimi sio mnafiki, tunapotaka kuweka vitu wazi, tuweke wazi,” alisema.

Aidha, Sallam sk alisisitiza kuwa hana ugomvi wowote na Harmonize na hata msanii huyo alipotaka kuondoka WCB na kwenda kuanzisha lebo yake, alimueleza jinsi gari anaweza kufanikiwa.


Post a Comment

0 Comments