Shirika la Mpango wa chakula duniani kutuma tani 50,000 za unga Lebanon

Ripoti ya ofisi ya Umoja wa Mataifa ya uratibu wa masuala ya kiutu iliyotolewa leo Jumanne imesema kuwa shirika la mpango wa chakula dunia WFP litatuma tani 50,000 za unga wa ngano mjini Beirut.

Msaada huo unajiri baada ya ripoti ya shirika la habari la Reuters kuonyesha kuwa serikali ya Lebanon haikuwa na nafaka ya kutosha kabla ya kutokea kwa mlipuko mkubwa katika mji huo wa bandari. Vile vile, maghala yote ya kibinafsi yaliokuwa yakihifadhi nafaka yaliharibiwa katika mlipuko huo

Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa unga huo utapelekwa ili kuhakikisha hakutatokea uhaba wa chakula nchini humo.Akiba ya unga ulioko kwa sasa inakadiriwa kukidhi mahitaji ya wiki sita pekee.

Post a Comment

0 Comments