Tetesi za soka Kimataifa

Nahodha wa Aston Villa Jack Grealish, 24, atapewa mkataba mpya wa pauni 100,000 wiki moja baada ya Manchester United kuonesha haina nia ya kutaka kumsajili. (Sun)

Manchester City bado haijawasiliana na Barcelona kuhusu beki wa kulia Sergi Roberto, licha ya kuhusishwa kwa kiasi kikuwa na mchezaji wa kimataifa wa Uhispania, 28, na haina mpango huo. (Manchester Evening News)

Mabingwa wa Ligi ya Premier Liverpool inakaribia kumaliza mkataba wa pauni milioni 9 kwa mlinzi wa Aissa Mandi wa Real Betis na Algeria, 28. (Bein Sports via Daily Mail)

The Reds pia inajitayarisha kwa dau la pauni milioni 10 kwa beki wa kushoto wa Norwich na Ireland Kaskazini Jamal Lewis, 22, wakati inatafuta nani wa kuvaa viatu vya Andy Robertson. (Daily Mirror)

Kiungo wa kati wa Southampton raia wa Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, 24, amepangiwa kujiunga na Tottenham kwa pauni milioni 15, huku beki wa Uingereza Kyle Walker-Peters, 23, akipata mkataba wa kudumu wa pauni milioni 12. (Telegraph)

Liverpool, Crystal Palace na Wolves wameonesha nia ya kumsajili winga wa Senegal, 22, Ismaila Sarr kutoka Watford iliyoshushwa daraja. (Watford Observer)

Leicester City wamefanya mazungumzo na Barcelona kuuliza ikiwa inaweza kumchukua mshambuliaji wa Ureno, 20, Francisco Trincao kwa misimu miwili ya mkopo, ikiwemo wajibu wa kumnunua kwa pauni milioni 45 (€50m) mwisho wa msimu. (Guardian)

Everton haitamsajili somo wake Everton kwa kuwa mshambuliaji huyo, 24, wa Brazil ameonekana kuwa tayari kujiunga na Benfica ya Ureno kutoka Gremio. (Goal)


Aliyekuwa beki ya kulia wa Chelsea Branislav Ivanovic anasema kuna uwezekano akawasiliana na aliyekuwa kocha wake Carlo Ancelotti akiwa Everton. (Sun)

Southampton imeonesha nia ya kumsajili mlinzi wa Groningen, Deyovaisio Zeefuik, 22, lakini mholanzi huyo anaaminika anapendelea kuhamia Ujerumani. (Southern Daily Echo)

Mshambuliaji wa Queens Park Rangers Eberechi Eze, 22, anamezewa mate na mahasimu wao wa London Crystal Palace na West Ham, huku kilabu hiyo inayoshiriki Ligi ya Mabingwa ikiweka thamani ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Under-21 kuwa pauni milioni 20. (Evening Standard)

Aliyekuwa kiungo wa kati wa Manchester United Angel Gomes, 19, amejiunga na klabu ya Ufaransa ya Lille kwa mkataba wa miaka mitano baada ya kuondoka Old Trafford msimu huu. (Metro)

Newcastle inammezea mate mshambuliaji wa Bournemouth raia wa Norway Josh King, 28, na kiungo wa kati wa Welsh David Brooks, 23, baada ya Cherries kushushwa daraja. (Telegraph)

Post a Comment

0 Comments