Ushauri maalumu kwa wanaume kuhusu wanawake katika kunogesha mahusiano ya kimapenzi


1. Mwanamke sio rula iliyonyooka kwamba hakosei, bali anapokosea adhabu yake si ngumi bali ni mawaidha.

2. Usihuzunike mkeo hapendezi au hanukii hali ya kuwa hujanunua nguo wala perfume ,wewe ndiye ulaumiwe.

3. Usifichue udhaifu wa mkeo kwa familia na marafiki zako. Itakurudia. Wewe ni mlinzi wa mkeo, naye ni mlinzi wako.

4. Usimkataze mkeo kushika simu yako baada ya kuita kwa kuiwahi wewe kabla hajaona anayekupigia, unachokichukulia tahadhari kikigundulika ndoa yenu itapata mitikisiko.

5. Usiogope kuchekwa kwa kumsaidia mkeo shughuli za ndani, mke si mtumwa isipokuwa ni msaada kwako.

6. Usipendepende kusifu wanawake wengine mbele yake, hujui maisha yao halisi yalivyo. Ukiibomoa hadhi yake, upendo wake kwako utashuka.

7. Usimgombeshe mkeo kwa kutoweza kupika vyakula unavyovipenda ,kwao hakukua na chuo cha upishi alipika kulingana na kinachopatikana, bora ni kumfundisha.

8. Usimpe mtu mwingine fursa ya kumhudumia mkeo, watu wanawaweza kufanya mambo mengine, lakini huduma za mkeo ni jukumu lako mwenyewe.

9. Hakuna mwanamke ambaye atamvumilia mwanaume dhaifu kitandani ,tumia kiwiliwili chako vizuri.

10. Peracetamol na dicloper isiwe ndio tiba ya kila ugonjwa anaoumwa mkeo ,suala la kumtibu ni lako usilikwepe.

11. Usiruhusu marafiki zako kuwa karibu mno na mkeo.

12. Usimlinganishe mkeo na wanawake wa nje hao hawajui thamani yako ,ukiendelea na hilo mapenzi ndani yatapungua.

13. Muheshimu mkeo hata kama wewe ndio mkuu wa familia kwani heshima ndio msingi wa ndoa yenu.

14. Usiwe mume mwenye dhana potovu juu ya mke ,uwaminifu ndidi ya mkeo ndiyo chanda njema.

15. Usimkosoe mkeo hadharani anapokosea ,hakuna anayekubali kukosolewa hadharani ,matoke ya hilo siku zote huwa hasi.

16. Maamkizi mema yapambanishwe na kugusana miili yenu ,jambo hilo huondoa madoa yaliyo katika nafsi zenu.

17. Neno "nakupenda" litawale kumwambia mkeo kwani mwanamke hufurahi kuambiwa neno hilo.

18. Penda kumshirikisha mkeo katika mipango ya kimaendeleo, mwanamke ni mshauri mzuri.

19. Watoto ni watoaji nje kila habari iliyo ndani kwenu, hivyo sehemu ya kumkosoa ni chumbani si mbele ya watoto.

20. Usimlaumu mkeo kwa kumkuta akiwa hayuko katika hali ya usafi, sms pia ingetosha kumjulisha kwamba unakuja ili ajiandae.

21. Wazazi unatakiwa kuwafanyia wema lakini usijisahau kiasi cha kusahau wajibu wako kwa mkeo ,uadilifu wako ndio utakaofanya wawili hawa waishi kwa upendo.

22. Usisahau kuwa mke anahitaji mtu anayemakinika naye na kumsikiliza vizuri, hivyo unapozungumza naye usiwe kama kamanda wa polisi, Mawasiliano yenye utulivu ndiyo msingi wa nyumba yenye furaha.

23. Iwapo mawazo yeke hayakufanikisha jambo kuliko mawazo yako, usimpuuze Bali ishini na mfanye kazi kama timu.

24. Maskani na vibaraza sio katika misingi ya ndoa ,kaa na mkeo ,mwanamke hupenda kumuona mwenza wake mara kwa mara.

25. Mfanyie suprise mkeo hata kwa chokolate ,hilo litaamsha hisia zake na kujiona unamjali.

26. Usisuhubiane na wanaume wenye mtazamo hasi na wa kimakosa kuhusu ndoa, kwani wavurugaji wa ndoa za watu ni binadamu wa kawaida,ulinzi wa ndoa yako ni jukumu lako.

27. Kumuoa wewe mkeo sikuvunja undugu wao panapo haja mpe ruhusa akawasamilie ndugu zake.

28. Umri au kuoa mke mwingine isiwe kikwazo cha kuwa na ushawishi kwenye nyumba yako.

29. Kamwe usipunguze kiwango cha huduma kwa familia yako kwa hali yoyote ile. Ifanye huduma yako kuwa yenye kujaa ubunifu maridhawa.

30.Wewe ndiye utakwenda kuulizwa mbele ya Mola muumba ,usimamizi wa ibada katika familia ni jukumu lako.