Uwezekano mkubwa wa wimbi la pili la maambukizi ya Corona Ufaransa

Wimbi la pili la janga la virusi vya corona , linaonekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kutokea nchini Ufarasa mwishoni mwa mwaka huu , ama katika majira ya baridi, chombo cha juu cha kisayansi kimeonya leo, wakati maafisa wakitafuta udhibiti wa ongezeko la kesi za maambukizi katika wiki mbili zilizopita.

Baada ya hatua za kuwazuwia watu kusalia majumbani mwao kupunguza viwango vya maambukizi, mataifa mengi ya Ulaya kwa sasa yanashuhudia tena ongezeko la maambukizi, ikiwa ni matokeo ya kulegeza vizuwizi na kujaribu kudhibiti uharibifu wa uchumi na kuruhusu watu wengi kuchanganyika katika msimu huu wa mapumziko.

Kamati ya kisayansi ya Ufaransa imesema katika taarifa iliyochapishwa na wizara ya afya kuwa hali ni tete na inawezekana wakati wowote kuingia katika hali ambayo itakuwa na udhibiti mdogo.