Loading...

Aug 3, 2020

Yanga yatoa orodha ya wachezaji 14 wanaoondoka kwenye kikosi

Uongozi wa Timu ya yanga umetoa orodha  ya wachezaji 14 wanaoondoka na 17 wanaobaki kwenye kikosi kwa ajili ya msimu ujao.

Wachezaji ambao wameachwa huru baada ya mikataba kuisha ni pamoja na Mrisho Ngassa, David Molinga, Jafary Mohammed, Tariq Seif, Andrew Vicent, Nahodha Papy Kabamba Tshishimbi, Mohammed Issa 'Banka.'

Wachezaji ambao Klabu inazungumza nao ili kusitisha mikataba yao ni Ali Mtoni, Muharami Issa Maundu, Ali Ali, Yikpe Gislain, Patrick Sibomana, Eric Kabamba na Rafael Daud.

Wachezaji ambao wanabaki kuendelea kuitumikia timu ya Wananchi ni Farouk Shikhalo, Ramadhan Kabwili, Metacha Mnata, Haruna Niyonzima, Lamine Moro na Bernard Morrison.

Wengine ni Feisal Salum, Juma Mahadhi, Adeyum Saleh, Said Juma Makapu, Balama Mapinduzi, Deus Kaseke, Ditram Nchimbi, Abdullaziz Makame na Paul Godfrey.

Aidha Klabu inaendelea na mazungumzo na wachezaji wake wakongwe, Juma Abdul na Kelvin Yondani ambao mikataba yao imeisha
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger