CCM Lindi wamvaa Membe, wasema amechemka kufanya kampeni


 

Na Ahmad Mmow, Lindi.

Kitendo cha mgombea wa urais anayepitia chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo), Bernard Membe kutoendelea kufanya mikutano ya kampeni kimetajwa kuwa ni dalili ya kushindwa kumudu gharama za uchaguzi.

Hayo yameelezwa leo na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wa wilaya ya Lindi, Abdallah Madebe kwenye mkutano wa kampeni ya udiwani wa kata ya Makonde, halmashauri ya manispaa ya Lindi.

Madebe ambaye alimsema mgombea huyo hafai kuchaguliwa kuwa Rais, alisema kitendo cha Membe kuzindua kampeni zake nakushindwa kuendelea ni dalili ya kushindwa kutokanana uwezo mdogo wa kumudu gharama za uchaguzi. Kwahiyo wanachama na wapenzi wa ACT- Wazalendo hawana budi kukubali kwamba mgombea wao amejitoa kimyakimya kwenye mbio za urais.

" Alizindua kampeni hapa Lindi akalala mbele, akaenda Dubai. Aliporudi akatangaza ataendelea na kampeni tarehe 17 mwezi huu, lakini hadi sasa hajaanza ameambiwa gharama ya kuendesha kampeni ya urais ni shilingi bilioni nne na wàbunge na udiwani bilioni kumi na saba waliomdandanya kwamba kugombea urais ni rahisi wamemwambia aweke mzigo wa bilioni ishirini na moja amechemka," alisema Madebe.

Mwenyekiti huyo alisema mgombea huyo alifanya uamuzi wa kujiunga na kugombea urais kupitia ACT-Wazalendo bila kutafakari. Nakwamba kabla ya kuchukua uamuzi huo alitakiwa amuulize aliyekuwa mgombea wa urais kupitia CHADEMA mwaka 2015, Edward Lowassa.

Mbali na hayo Madebe alitoa wito kwa wananchi wa Lindi wasimpigie kura Membe. Kwamadai kwamba ni mbinafsi na hana uzalendo. Kwani hata barabara kwa kiwango cha lami amejenga kuanzia kijiji cha Rutamba mpaka nyumbani kwake Rondo Chiponda badala ya Ngongo.

Alisema Membe licha ya kuishi Ulaya miaka 12 hakuisaidia Lindi. Lakini pia alikuwa mbunge wa jimbo la Mtama kwa vipindi vitatu lakini katika kipindi chake cha ubunge hakufanya jambo lamaana na lenye faida kwa wananchi wa Mtama. Badala yake alidumaza jimbo hilo.

" Serikali ilitenga msitu pale Rondo, lakini umeharibiwa. Yote hayo yamefanyika wakati yeye yupo na alikuwa anaangalia tu. Hata hoteli amejenga Mtwara badala ya Lindi. Kiwanda cha saruji ambacho fedha zilitolewa na Ghaddaf  hakijajengwa. Huyo anafaa kuwa Rais?," Madebe alizidi kumvaa Membe.

Kiongozi na kada huyo wa CCM wilaya ya Lindi alisema Watanzania wanatambua kwamba anayetosha kuwa Rais ni Rais aliye madarakani,Dkt John Magufuli kwani amepandisha uchumi, amerejesha nidhamu kazini na miradi mingi ya maendeleo inatekelezwa kwakutumia mapato ya ndani.

Post a Comment

0 Comments