Diwani Mstaafu Rissa azindua kampeni ,ahaidi kuwaletea wananchi maendeleo



Na Timothy Itembe Mara.

Mgombea udiwani kata ya Kitembe ndani ya halmashauri ya Rorya mkoani Mara, Thomas Patrrick Rissa katika uzinduzi wa mkutano wa kampeni ametaja sababu za kuomba wananchi ridhaa ya kumchagua 2020 ili kuwatumikia.

Rissa amesema kuwa sababu kubwa iliyomsukuma ni  kuwaletea wananchi wa kata ya Kitembe maendeleo tofauti na watangulizi wake waliopita na kumtangulia kwenye nafasi hiyo.

Rissa amejigamba kukamilisha na kutekeleza miradi ndani ya kata yake kwa pindi cha uongozi wake tofauti na waliomtangulia ambapo amedai kuwa hayo alifanikiwa kwasbabu ya kujenga  mahusiano mazuri baina ya Halmashauri kwa kushirikiana na madiwani wenzake pamoja na watumishi.

Mgombea huyo aliongeza kuwa  Wananchi wake  wakiona vyema kwa maendeleo aliyowaletea kwa miaka mitano wataende kumpa kura nyingi za kutosha 2020-2025   kumpeleka halmashauri kuwatumikia  na kukamilisha baadhi ya miradi lengwa aliyoianzisha.

 “Ndani ya kata ya Kitembe kwenye uongozi wangu nimetekeleza miradi mingi ikiwemo kujenga Zahanati mpya ndani ya kijiji cha Kitembe ili kusogeza huduma karibu na Wanachi,Barabara ya kuunganisha Nyambori  na Nyambogo,Nyambogo-Raranya na kitembe hadi Osiri(Kata ya Roche),Huduma ya maji safi na salama ambayo inapatikana katika kijiji cha Nyambogo”alisema Rissa.

Mafaniko mengine ni pamoja na Uboreshaji wa barabara za kutoka Ryagoro Ingiri juu(Makao makuu ya wilaya) kwa lengo la kumarisha usafiri na usafirishaji ndani ya kata hadi barabara kuu toka Shirati kwenda  wilayani Tarime kwa kupitia kata ya Roche.

Katika sekta ya Elimu Diwani mstaafu,Thomas Patrrick Rissa alisema kuwa amefanikisha kuanzishwa shule mpya ya Sekondari inayojengwa katika kijiji cha Nyambogo ilikuwaondolewa wanafunzi adha ya kutembea mwendo mrefu kufuata masomo katika shule ya sekondari Charya na kupunguza changamoto ya uwezekano wa wanafunzi wa kike kupata mimba zisizotarajiwa.

Pia Rissa katika upande wa Elimu alimaliza kwa kusema kuwa kipindi chake wamefanikiwa kuongeza vyumba 3 kimoja shule ya kitembe na 2 shule ya msingi Dagopa huku wakifaulu kuchimba matundu ya choo Dagopa matundu 6 Kitembe matundu 10 ikiwemo kukarabati vyumba vya madarasa ndani ya kata hiyo.

Naye Joseph Oseyo Mwenyekiti msataafu kitongoji cha Misiri alikiri kuwepoa mafanikio kipindi cha uongozi wa diwani huyo ambapo alisema kuwa kumekuwepo na frusa mbalimbali ikiwemo kukaribisha taasisi mbalimbali kama vile taasisi ya Village life out rich Project (V.E.L.P).

Oseyo aliongeza kuwa Taasisi hiyo imewachimbia kisima cha maji na wanapata maji safi na salama ndani ya kata ya Kitembe na kuwa Taasisi hiyo imefanikiwa kujenga kituo cha Afya katani hapo ili wananchi wapate huduma karibu.

Pia Oseyo alimaliza kwa kusema kuwa diwani emapambana na wizi wa mifugo katika kipindi chake chote cha uongozi ambapo wizi huo umepungua na wananchi sasa wanalala na wengine wameongeza watoto kwani kabula ya  hapo nyuma wizi ulikuwa ukishika kasi ambapo wananchi hususani vijana wamekuwa wakitumia nguvu na mda mwingi  kufuata bila kukaa na familia zao jambo ambalo kwasasa limepungua.  

Mery Wilyam alisema kuwa amefanya kazi kubwa ya maendeleo kwa ushirikiano wa diwani Rissa kwa hali hiyo wananchi na wapiga kuwa kwa ujumla wamchague ili kukamilisha yale ambayo yamebakia pia alitimia nafasi hiyo kuwaomba wapiga kura kumchagua mgombea urais wa Chama chake,Tundu Risu na diwani anayetokana na Chadema ili kujipatia maendeleo. 

Post a Comment

0 Comments