https://monetag.com/?ref_id=TTIb Kimbaki afunika wakati wa kurudisha fomu ya NEC ya kuteuliwa kugombea Ubunge jimbo la Tarime Mjini | Muungwana BLOG

Kimbaki afunika wakati wa kurudisha fomu ya NEC ya kuteuliwa kugombea Ubunge jimbo la Tarime Mjini

 


Na Timothy Itembe Mara.

MAMIA ya wanachama wa cha mapinduzi CCM pamoja na wananchi wa Tarime na viungo vyake wamejitokeza jana kumsindikiza Michael Kembaki katika mchakato wa kurudisha  Fomu ya Tume ya uchaguzi NEC ili kuteuliwa kuwa  mgombea ubunge jimbo la Tarime mjini ili akipambana na wagombea wa vyama pinzani watako kuwa wameteuliwa.

 Mgombea Ubunge Jimbo la Tarime mjini Michael Kembaki anaonekana kukubalika kipindi hiki tofauti na kipindi kilichopita cha uchaguzi wa mwaka 2015 kutokana na kutimiza ahadi alizoahidi kwa Wananchi wa halmashauri ya Mji wa Tarime  wakati akigombea nafasi hiyo  licha ya kuwa kura hazikutosha ambapo alichaguliwa Esther Matiko wa Chama cha Demokorasia na maendeleo Chadema.

Akikabidhi fomu kwa Afisa uchaguzi halmashauri ya Mji wa Tarime mjini,Elias Ntiruhungwa mgombea huyo alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua na kuwa Mbunge  katika jimbo hilo ili kutimiza adhima ya kuwaletea Wananchi  maendeleo.

Kembaki aliwataka wananchi kwa ujumla kumwamini na Chama chake pindi mchakato wa kupiga kura utakapofika kumchagua na Mgombea Urais DR John Pmbe Magufuli kwasababu chama chake kimetekeleza ahadi ya maendeleo kwa wananchi wake.

Kwa upande wake Katibu wa Chama hicho wilaya Tarime,Khamis Mkaruka alisema kuwa wamejipanga kushinda nafasi ya Urais pamoja na majimbo yote mawili jimbo la Tarime Mjini analo gombea Michael Kembaki pamoja na jimbo la Tarime vijijini analogombea Mwita Mwikwabe Waitara na kuwa hana mashaka wananchi watakipigia kura chama chake.

Pia Katibu huyo aliongeza kuwa chama chake kupitia Rais Magufuli kimetekeleza Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015 na kuwa kutokana na utekelezaji huo wa miradi kwa jamii wagombea wake wanajiuza.

Mkaruka aliomba waumini na wafuasi wa vyama vya siasa wakiwemo wagombea kufanya kampeni za kistaarabu ili kuepuka kufanya kampeni zenye fujo na kuvuruga Amani tuliyoachiwa na mtanguzi wetu Baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Wakati huohuo Mgombea Unge jimbo la Tarime vijijini kupitia Chama cha mapinduzi Mwita Mwikwabe Waitara jana amerudisha fomu ya NEC ya kuteuliwa kuwa mgombea jimbo la Tarime vijijini ili kupambana na John Heche wa Chadema.

Post a Comment

0 Comments