Koka ahaidi neema kwa wafanyabiashara wa soko la Loliondo Kibaha mjini

 


Mgombea huyo aliyasema hayo wakati wa wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya maili moja vilivyopo Kibaha mji ambao ulihdhiliwa na viongozi mbali wa chama cha CCM pamoja na wananchi kutoka maeneo mbali mbali.

Koka aliongeza kuwa katika kipindi kilichopita aliweza kushirikiana na serikali ya awamu ya tano katika kufanikisha miradi mbali mbali ya maenedeleo na kwamba aliweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kupeleka maombi yake ambayo kwa kiasi kikubwa yaliweza kuzaa matunda baada ya kukubaliwa kupata mradi mkubwa wa ujenzi wa soko la kisasa ambalo limeshaanza kujengwa.

“Kikubwa ambacho ninawaomba wananchi wenzangu wa jimbo la Kibaha mji naombeni kwa moyo mkuchufu kuweza kuniamini tena katika kipindi kingine ni mwakilishi wenu katika bunge ii niweze kusikiliza changamoto zenu mbali mbali amabzo zinawakabili ili niweze kuzitafutia ufumbuzi kwa kushirikiana na serikali,”alisema Mgombea huyo.

Aidha alisema kwamba anatambua kuna baaadhi ya wafanyabishara wanafanya kazi zao katika mazingira magumu na wengine hawana eneo maalumu kwa ajili ya kufanyia shughuli zao za biashara mbali mbali ivyo lengo lake kubwa ni kuhakikisha ananweka mipango madhubuti ambayo itasaidia kuendesha biashara bila ya kuwepo kwa usmbufu wowote.

“Mimi kwa kweli nina imani kuna mambo mengi ambayo nimeweza kuyatekeleza wakati wa kipindi changu cha Ubunge kwa hiyo ninaomba wananchi wa Jimbo la Kibaha mjini tuendelee kushirikiana bega kwa bega ili miradi mingine ambayo bado haijakamilika iweze kukamilika na nina imani kubwa soko ili kubwa la kisasa pindi likikamilika litaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa wafanyabiashara,”aliongeza Koka.

Katika hatua nyingine mgombea huyo alisema kwamba serikali ya awamu ya tano ambayo inaongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli imeweza kufanya mambo makubwa kutokana na kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ambayo itaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa wananchi ambao walikuwa wanakabiliwa na changamoto mbali mbali.

Kwa upande wake Mke wa Mgombea huyo Mama Selina Koka hakusita kuwaomba wananchi wa Jimbo la Kibaha mjini kuweza kumpata nafasi nyingine mume wake ili aweze kushirikiana kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo lengo ikiwa  kupiga hatua zaidi  katika sekta mbali mbali.

“ Kwa heshima kubwa kwa kweli naweza nikasema serikali ya awamu ya tano imeweza kufanya mambo mengi sana lakini kitu kikubwa naomba muendelee kumuamini mume wangu aweze kupata kura nyingine katika uchaguzi mkuuu ambao unatarajiwa kufanyika Octona 28 mwaka huu hivyo imani yangu mtaweza kumpatia kura nyingine za ndio,”alisema Mama Selina Koka.

Naye  aliyekuwa mmoja wa wagombea katika nafasi ya Ubunge jimbo la Kibaha mjini katika hatua  ya mchakato wa kura za maoni Waziri Manyakala alibainisha kwamba kwa sasa nia yao ni moja na kwamba tofauti zote wameshazoweka pembeni  kwa lengo la kuweza kuwa kitu kimoja na kushirikiana ili kuweza kuleta maendeleo ya pamoja.


Post a Comment

0 Comments