Majaliwa awataka Wagombea Udiwani na Ubunge Manyara kurejesha Mashamba kwa wananchi


Na John Walter-Manyara

Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amezindua kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Manyara kuelekea Uchaguzi Mkuu waOktoba 28.

Uzinduzi huo uliohudhuriwa na mamia ya wakazi wa Mkoa huo, ulifanyika mjini Babati katika Uwanja wa Kwaraa.

Viongozi mbalimbali wa serikali na Chama ni miongoni mwa waliofurika katika uzinduzi huo.

Majaliwa katika hotuba yake alisema serikali ya chama cha Mapinduzi imefanya mengi na kwamba kwa sasa ina  mpango wa kukamilisha miradi ambayo haijakamilika na kuanzisha miradi mipya itakayoifanya Tanzania kuwa nchi dhabiti ikiwa watachaguliwa tena.

Waziri Mkuu aliwataka wagombea Udiwani na Ubunge kuhakikisha wanarudisha mashamba yote ya wawekezaji yasiyoendelezwa na kupewa wananchi waweze kulima na kujenga.

Mwaka 2020 Magufuli atapambana na wagombea urais wengine 14 huku Watanzania 29.2 milioni waliojisajili kupiga kura wakitarajiwa kushiriki zoezi hilo ikilinganishwa na 23 milioni waliojisajili mwaka 2015.

Chama cha Mapinduzi mkoa wa Manyara kina wagombea saba katika Majimbo ya Mbulu Mjini na Vijijini,Babati Mjini na Vijijini, Simanjiro, Hanang na Kiteto.

Mgombea Ubunge Jimbo la Babati mjini Paulina Gekul ambaye alichukua hatamu za uongozi  2015 akiwa Chama kikuu cha Upinzani nchini (CHADEMA)  anawania nafasi  hiyo akitafuta muhula wa pili.

Jimbo la Mbulu, Wabunge waliomaliza muda wao Flatey Masay wa Mbulu Vijijini na Zakaria Isaay  wa Mbulu Mjini wamerejea kwenye kinyang'anyiro.

Jimbo la Hanang anagombea Eng Samuel Hhayuma aliepishwa na Dr.Marry Nagu wakati Jimbo la Kiteto mgombea  ni  Wakili Edward Ole Lekaita na Simanjiro anagombea aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher  Ole Sendeka

Post a Comment

0 Comments