Malefu ya watu wakimbia nyumba zao kufuatia moto wa nyika


Makumi kwa maelfu ya watu jimboni California wamekimbia nyumba zao baada ya kutokea kwa moto wa nyika katika maeneo ya Napa na Sonoma.Maafisa wa dharura wamesema watu watatu wamekufa wakati moto ulipozuka kaskazini mwa jimbo hilo.

Kwa mujibu wa maafisa wa idara ya wazima moto, baadhi ya mashamba ya mizabibu katika eneo la Napa yaliteketea kwa moto ambao ulienea kwa zaidi ya ekari 35,000.

Mkuu wa idara ya wazima moto katika jimbo hilo Tony Gossner amesema kampuni maarufu za mvinyo kama vile Chateua Boswell pia ziliteketea kwa moto huku majengo kadhaa pia yakiharibiwa.

Mamlaka imeamuru zaidi ya watu 35,000 kuhama makaazi yao wakati moto huo ukitarajiwa kuenea kwa kasi.Uchunguzi wa kubaini chanzo cha moto huo bado unaendelea.

Post a Comment

0 Comments