Marekani kupinga mamlaka ya mahakama ya ICJ kuhusu kesi ya Iran

 

Mawakili wa Marekani wanatarajiwa leo Jumatatu kupinga mamlaka ya mahakama ya juu zaidi ya Umoja wa Mataifa kutatua kesi iliyowasilishwa na Iran ikitaka kuondolewa kwa vikwazo ilivyowekewa na Marekani.

Iran iliwasilisha kesi katika mahakama ya kimataifa ya haki ICJ, ambayo pia inafahamika kama Mahakama ya dunia mwaka 2018 ikiitaka mahakama hiyo kuiagiza Marekani kuondoa vikwazo dhidi ya Iran kwa sababu Washington ilikiuka mkataba wa urafiki wa miongo kadhaa.

Hata hivyo Marekani imesisitiza kuwa lengo halisi la Iran kuwasilisha kesi hiyo ni kuurejesha mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 uliopingwa na utawala wa Rais Donald Trump.

Iran inahoji kwamba vikwazo hivyo, vilivvyowekwa na Marekani, baada ya kujitoa kwenye makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015, ambayo yalilenga kuizuia Tehran kutengeza silaha za nyuklia, vinakiuka mkataba wa mwaka 1955 wa urafiki baina ya nchi hizo mbili.

Baada ya Iran kuwasilisha kesi mbili kwa msingi wa mkataba huo dhidi ya Marekani katika mahakama ya ICJ, Marekani ilitangaza kujiondoa rasmi katika mahakama hiyo, lakini hatua hiyo hakuathiri kesi inayoendelea.

Post a Comment

0 Comments