Meli ya Alan Kurdi ya Ujerumani yawaokoa wahamiaji 133

 


Shirika la msaada wa kibinadamu la Ujerumani, Sea-Eye, limesema jana kuwa meli yake ya uokoaji ya Alan Kurdi imewaokoa wahamiaji 133 waliokuwa wanajaribu kufika barani Ulaya kupitia bahari ya Mediterrenia. 


Shirika hilo limesema kuwa awali meli hiyo iliwaokoa takriban watu 114 kutoka mashua moja ya mbao.Miongoni mwa wale walioathirika ni watoto wanane na wanawake wanane ambapo mmoja alikuwa mjamzito. 


Katika ujumbe kupitia mtandao wa twitter, shirika hilo la Sea-Eye limesema kuwa wahudumu wa meli hiyo ya Alan Kurdi waliwaokoa watu 19 kutoka kwa boti la uvuvi waliowajumuisha wanawake wanne na watoto 10 na kuifanya idadi jumla ya watu waliookolewa katika meli hiyo kufikia 133. 


Mwenyekiti wa shirika la Sea-eye, Gorden Isler, amesema kuwa wahamiaji hao walikuwa na bahati sana kupatikana na wahudumu wa meli hiyo na kwamba walinzi wa Pwani ya Libya na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM, awali hawakuzungumzia kuhusu uokoaji huo.

Post a Comment

0 Comments