Miili ya watoto 10 haitambuliki- Kamati ya ulinzi


 Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Kagera imefika eneo la tukio katika shule ya Msingi Byamungu Islamic eneo ambapo wanafunzi kumi wamefariki baada ya Bweni lao kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Revocatus Malimi amesema miili ya Wanafunzi hao imeshindwa kutambulika kwasababu imeharibika sana "kinachofanyika itachukuliwa vinasaba miili hiyo pamoja na Wazazi wao ili waweze kutambulika na taratibu za mazishi zifanyike"

Post a Comment

0 Comments