https://monetag.com/?ref_id=TTIb Misri yagundua makaburi 14 ya kale katika eneo la Saqqara | Muungwana BLOG

Misri yagundua makaburi 14 ya kale katika eneo la Saqqara

 


Wizara ya mambo ya kale ya Misri imetangaza leo kupatikana kwa majeneza 14 katika eneo la Saqqara ambayo yamezikwa kwa muda wa takriban miaka elfu mbili na nusu.


Katika taarifa yake, wizara hiyo imesema kuwa makaburi hayo yalipatikana siku mbili zilizopita wakati wa shughuli ya uchimbaji wa akiolojia na hii inafuatia kupatikana kwa aina ya masanduku kama maiti, yaliochongwa kwa mbao katika eneo hilo la makaburi wiki iliyopita. 


Eneo hilo la Saqqara lililo kusini mwa nchi hiyo ni sehemu ya mji mkuu wa kale wa Memphis na limo kwenye Turathi za Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni, UNESCO. 


Misri inataka kukuza uvumbuzi wa akiolojia kote nchini humo kwa lengo la kufufua utalii, ambao ulipata pigo huku kukiwa na vikwazo vya kusafiri kwa sababu ya janga la virusi vya corona.

Post a Comment

0 Comments