Mkuu wa EU asema matumaini ya makubaliano ya kibiashara ya Brexit yafifia kila kukicha

 


Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen ameionya Uingereza kuwa imesalia na muda mchache kabla mwisho wa mwaka huu kufikia maelewano ya kibiashara na Umoja wa Ulaya. 

Katika hotuba yake ya sera ya kila mwaka von der Leyen amezisisitizia Umoja wa Ulaya na Uingereza kujadiliana kwa haraka na kufikia maelewano akionya kwamba makubaliano ya Brexit hayawezi kubadilishwa au kutupiliwa mbali. 

Amelizungumzia suala hilo la Brexit kwa kifupi huku umuhimu mkubwa akiuweka katika jinsi Umoja wa Ulaya utakavyofufua uchumi wake baada ya janga la virusi vya corona. 

Amezungumzia kwa kirefu pia uwekezaji wa kidijitali pamoja na masuala kuhusiana na mazingira.


Post a Comment

0 Comments