Mwalimu Mkuu na Mhasibu waliokula hele za chakula cha wanafunzi warudisha

 

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kilimanjaro, Frida Wikesi amesema wamefanikiwa kurejesha Tsh. 2,600,000 kwa Kamati ya Shule ya Msingi Msasani iliyopo Wilayani Moshi.

Fedha hizo ambazo zilikuwa zinatolewa na wafadhili kwa ajili ya chakula cha mchana kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu, zilikuwa zinachepushwa na aliyekuwa Mkuu wa Shule hiyo akishirikiana na Mwalimu aliyekuwa Mhasibu wa Shule.

Ilibainika kuwa kwa mwaka 2016, 2017 na 2018 fedha hizo zilikuwa zikiingia lakini Mkuu wa Shule alikuwa hazifikishi kwenye Kamati ya Shule bali anazitumia kwa matumizi binafsi.

TAKUKURU ilitoa wito kuwa fedha hizo zitumike kwa matumizi sahihi ya wanafunzi. Pia, imetoa wito kuwa fedha za wahisani au michango ya wazazi ziwe zinapelekwa kwa Kamati husika.

Post a Comment

0 Comments